Lugha: Kiswahili | Kiingereza | Kinorwei

Nairobi 
Langata Road, P.O. Box 24569, 00502 Karen, Nairobi, Kenya
Barua pepe: nlmear@nlm.no

Scripture Mission Conference Center (SMCC)
Conference Centre Manager: +254 728 961 984
E-mail: nlmear.smcc@nlm.no

Kristoffer Krohn Sævre - Mkurugenzi
Simu: +254 727 847 004
Barua pepe: nlmostafrika@nlm.no

Nicholas Ondari - Meneja ya SMEA
Simu: +254 722 544 972
Barua pepe: nlmear.genman@nlm.no

Arusha
P.O. Box 2696
Arusha
Barua pepe: nlmear.arusha@nlm.no

Joakim Ami - Meneja
Mobile: +255 784 590 870


Voi
P.O.Box 100, Voi

Hezron Mwasi - Meneja
Simu: +254 721 460 694
E-mail: nlmear.voistation@nlm.no

Scripture Mission ni jina rasmi ya wamissionary wa Lutheran kutoka Norway (Norwegian Lutheran Mission NLM) katika Afrika Mashariki, hutumika katika sehemu ya kazi ya mission ambayo haichangamani na makanisa ya wenyeji ya kilutheri. Wito wa NLM ni Ulimwengu kw kristo.

Huduma ya redio
Huduma hii ya FEBA radio ilianza mwaka 1981,vipindi vinaandaliwa na wakenya katika studio ya Voi, wasikilizaji wengi kati yao hao ni Waislamu wakielezea juu ya kukutana na Yesu kwa kupitia mpango huu.

Huduma ya Maandiko
Kituo cha maandiko Arusha Tanzania wanahusika hasa na utoaji wa vitabu,usambazaji wa maandiko, kozi ya kujifunza Biblia kwa njia ya posta na elimu mbalimbali ya Kikristo.

Uongozi na shule ya bweni
Makao makuu ya Ofisi ya Mission ya NLM Afika Mashariki yako Nairobi Kenya, katika eneo hilo pia kuna shule ya watoto wa wamissionay,nyumba ya wageni na kituo cha mikutano.

Sehemu ya Makanisa ya wenyeji
Scripture Mission husaidia kazi za NLM katika sehemu zingine, zaidi Mission ya
NLM hufanya kazi pamoja na makanisa ya kiinjili ya kilutheri Kenya na Tanzania (ELCK, ELCT). NLM ilianzisha huduma yake huko Mbulu (Dongobesh) mwaka 1951, Mara mwaka 1972. Mwaka 1977 NLM walianza ushirikiano na kanisa la kilutheri Kenya.

NLM hutoa fedha za misaada kwa makanisa. Dayosisi wanawajibu katika huduma na itakuwa mhusika wa mambo muhimu na malengo. Wamisionari wa NLM wanayo kazi pamoja na uinjilisti, elimu na huduma ya Afya, Ndiyo maana Wamissionari ni sehemu ya huduma za makanisa, wote kwa pamoja tunahesabika ni wafanyakazi wa Taifa.

Tanzania NLM ina wamisionari wanaofanya kazi ya uinjilisti kati yakabila ya Wadatoga huko Mbulu, tuna wamisionari wengine katika eneo la pwani huko Kenya, Shule ya Biblia Kiabakari na kituo cha Biblia Kapenguria kwa sasa hatuna misionari yeyote ila NLM bado wanatoa msaada wa fedha. NLM wamejiingiza katika huduma ya afya kwakupitia Hosiptali ya Haydom huko Dayosisi ya Mbulu na Bunda Mara.

(Picha: Øyvind Stavnes)

Masomo kwa njia ya Posta – kwa bei za Masomo mnapata vitabu pia.

Badala ya Tshs. 200/= Masomo: Bure Jon Jøssang
Maneno haya mawili – Badala ya – ni ”ufunguo” wa kufahamu mengi katika Biblia. Badala ya ilikuwa mpango wa Mungu, na kwetu ni Habari Njema! Kitabu hiki kina maswali yanayopatikana kwa njia ya Posta.

Imani Yangu Tshs. 500/= Masomo: 300/= Gudmund Vinskei
Je, katika maisha yako, unaamini nini? Katika somo hili tunajifunza kuhusu msingi wa imani yetu ya kikristo. Ni somo muhimu kwa yule anayetaka kupima imani yake! Barua kumi za kujibu.

Maombi/Prayer Tshs. 1.000/= na 900/= Masomo: 500/= Ole Hallesby
Maombi ni safari ndefu, na wengi wanachoka njiani! Mafundisho haya yanatutia mayo na yanatuwezesha kuzungumza na Baba yetu wa mbinguni. Barua kumi na nne za kujibu.

Nayajua Matendo Yako Tshs. 400/= Masomo: 400/= Øyvind Andersen
Katika Ufunuo tunapata maneno ya Yesu mwenyewe kwamba anaona mwenendo wetu. Hatuwezi kuficha kitu kwake! Maneno haya ya Yesu yana maana kubwa kwa kili mtu. Barua nane za kujibu.

Tukaze Mwendo Tshs. 500/= Masomo: 300/= Fidon R. Mwombeki
Masomo haya yanatufundisha juu ya safari yetu ya Mbinguni jinsi ilivyo na magumu mengi. Mtume Paulo alisema nakaza mwendo ili nifikilie mede ya thawabu. Barua tano za kujibu.


Ujasiri wa Leo, Tumaini la Kesho Tshs. 2.500/= Esther Onstad
Katika fundisho hili la Ufunuo wa Yohana, mwandishi anaeleza mifano inayoonyesha mashindano kati ya Mungu na shetani na ushindi wa mtu wa Mungu. Mkazo wa Ufunuo ni ushindi wa Bwana Yesu Kristo anayeshinda kila adui na ambaye ataleta mbingu mpya na nchi mpya.

Uongozi wa Usharika Tshs. 3.500/= Fidon R. Mwombeki
Kazi ya uongozi ni ufundi! Mchungaji aliyesoma theolojia ana uwezo kutawala kazi zote za Usharika wake? Kitabu hiki kinawasaidia ”wenye nia ya kujihami mbinu za utawala ya kisasa.”

Wakristo Tuwe Macho Tshs. 500/= Masomo: 400/= Fidon R. Mwombeki
Mafundisho kuhusu ”Matendo ya Roho Mtakatifu”, jinsi yalivyoonyeshwa katika Waraka wa Galatia 5:22-23. Kozi hii inatufundisha juu ya mwenendo mzima wa mkristo anavyostahili kusihi katika maisha yake hasa juu ya tunda ya kiroho. Kitabu hiki kina maswali yanayopatikana kwa njia ya Posta. Barua nane za kujibu.

Dini na Maisha Tshs. 300/= Jon Jøssang
Somo hili linatuonyesha ni dini ipi iliyo ya kweli. Tukisoma kutoka Biblia, tunaona kwamba dini iliyo safi ni kwenda kuona wagonjwa na wenye matatizo. Hii ndiyo dini iliyo safi! Barua nane za kujibu.

Hekima/Wisdom Tshs. 500/= Prof. Pontoppidan
Kitabu hiki ni muhtasari wa majibu sahihi yanayotokana n a maswali mengi kuhusu imani na maisha ya kikristo.

Historia ya Kibiblia/A Shorter Bible History Tshs. 400/=
Kitabu kinachoelezea historia ya Biblia kwa maelezo machache.

Katika Moto wa Tanuru Tshs. 800/= Aud Sæverås
Ushuhuda wa kweli wa mkristo mmoja wa Ethiopia aliyeteswa kwa ajili ya imani yake ya Ukristo wakati wa ukomunisisti.

Katikati ya Majambazi Tshs. 800/= Marie Monsen
Kitabu kinachoeleza ushuhuda wa mama mmoja aliyefanya kazi ya Umisheni katika nchi ya China wakati wa vita.

Lisha Kondoo Zangu Tshs. 400/= Fritz Larsen
Msaada kuandaa mahubiri kutoka Injili nne za Agano Jipya.

Msingi wa Imani Tshs. 700/= Carl Fr. Wisløff
Mwongozo wa elimu ya imani za Ukristo.

Msingi wa Wokovu Tshs. 900/= Øyvind Andersen
Utangulizi wa Waraka wa Warumi 1-8

Njia ya Wokovu Tshs. 300/= Kai Pedersen
Kijitabu kinachofafanua juu ya wokovu wa Yesu Kristo.

Pastoral Care Tshs. 400/= Øyvind Eide
Mwonogzo wa elimu ya uchungaji wa kanisa. Kinapatikana kwa lugha ya kiingereza.

Roho Mtakatifu Enok Sørensen
Roho Mtakatifu ni wa muhimu sana kwa mkristo, kwani hutukumbusha udhaifu wetu mara kwa mara. Biblia inasema mengi kuhusu Roho Mtakatifu, na kozi hii inatufundisha juu ya maandiko haya.

Twende kwa nani? Mch. Fedon Mwombeki
Mtume Petro alikuwa wa kwanza kumkiri Yesu, lakini katika mateso alimkana. Hatimaye aliona Yesu ndiye njia ya kufika kwa Baba. Maisha yake Petro yana mafundisho muhimo hata kwa maisha yetu! Barua nane za kujibu.

Ubatizo wa Kikristo Svend Aage Jacobsen
Je kwanini tunabatizwa? Katika somo hili tunajifunza mengi juu ya ubatizo wa kikristo kama Yesu mwenyewe alivyotuagiza katika Mth 28:19. Barua saba za kujibu.Ukitaka habari zaidi kuhusu Scripture Mission na kazi yetu, waziliana nasi kwa anwani hii:

Scripture Mission. S.L.P. 2696, Arusha, Tanzania
Simu: (027) 250-8201
Barua pepe: arusha@scripture-mission.com