Masomo kwa njia ya Posta – kwa bei za Masomo mnapata vitabu pia.
Badala ya Tshs. 200/= Masomo: Bure Jon Jøssang
Maneno haya mawili – Badala ya – ni ”ufunguo” wa kufahamu mengi katika Biblia. Badala ya ilikuwa mpango wa Mungu, na kwetu ni Habari Njema! Kitabu hiki kina maswali yanayopatikana kwa njia ya Posta.
Imani Yangu Tshs. 500/= Masomo: 300/= Gudmund Vinskei
Je, katika maisha yako, unaamini nini? Katika somo hili tunajifunza kuhusu msingi wa imani yetu ya kikristo. Ni somo muhimu kwa yule anayetaka kupima imani yake! Barua kumi za kujibu.
Maombi/Prayer Tshs. 1.000/= na 900/= Masomo: 500/= Ole Hallesby
Maombi ni safari ndefu, na wengi wanachoka njiani! Mafundisho haya yanatutia mayo na yanatuwezesha kuzungumza na Baba yetu wa mbinguni. Barua kumi na nne za kujibu.
Nayajua Matendo Yako Tshs. 400/= Masomo: 400/= Øyvind Andersen
Katika Ufunuo tunapata maneno ya Yesu mwenyewe kwamba anaona mwenendo wetu. Hatuwezi kuficha kitu kwake! Maneno haya ya Yesu yana maana kubwa kwa kili mtu. Barua nane za kujibu.
Tukaze Mwendo Tshs. 500/= Masomo: 300/= Fidon R. Mwombeki
Masomo haya yanatufundisha juu ya safari yetu ya Mbinguni jinsi ilivyo na magumu mengi. Mtume Paulo alisema nakaza mwendo ili nifikilie mede ya thawabu. Barua tano za kujibu.
Ujasiri wa Leo, Tumaini la Kesho Tshs. 2.500/= Esther Onstad
Katika fundisho hili la Ufunuo wa Yohana, mwandishi anaeleza mifano inayoonyesha mashindano kati ya Mungu na shetani na ushindi wa mtu wa Mungu. Mkazo wa Ufunuo ni ushindi wa Bwana Yesu Kristo anayeshinda kila adui na ambaye ataleta mbingu mpya na nchi mpya.
Uongozi wa Usharika Tshs. 3.500/= Fidon R. Mwombeki
Kazi ya uongozi ni ufundi! Mchungaji aliyesoma theolojia ana uwezo kutawala kazi zote za Usharika wake? Kitabu hiki kinawasaidia ”wenye nia ya kujihami mbinu za utawala ya kisasa.”
Wakristo Tuwe Macho Tshs. 500/= Masomo: 400/= Fidon R. Mwombeki
Mafundisho kuhusu ”Matendo ya Roho Mtakatifu”, jinsi yalivyoonyeshwa katika Waraka wa Galatia 5:22-23. Kozi hii inatufundisha juu ya mwenendo mzima wa mkristo anavyostahili kusihi katika maisha yake hasa juu ya tunda ya kiroho. Kitabu hiki kina maswali yanayopatikana kwa njia ya Posta. Barua nane za kujibu.
Dini na Maisha Tshs. 300/= Jon Jøssang
Somo hili linatuonyesha ni dini ipi iliyo ya kweli. Tukisoma kutoka Biblia, tunaona kwamba dini iliyo safi ni kwenda kuona wagonjwa na wenye matatizo. Hii ndiyo dini iliyo safi! Barua nane za kujibu.
Hekima/Wisdom Tshs. 500/= Prof. Pontoppidan
Kitabu hiki ni muhtasari wa majibu sahihi yanayotokana n a maswali mengi kuhusu imani na maisha ya kikristo.
Historia ya Kibiblia/A Shorter Bible History Tshs. 400/=
Kitabu kinachoelezea historia ya Biblia kwa maelezo machache.
Katika Moto wa Tanuru Tshs. 800/= Aud Sæverås
Ushuhuda wa kweli wa mkristo mmoja wa Ethiopia aliyeteswa kwa ajili ya imani yake ya Ukristo wakati wa ukomunisisti.
Katikati ya Majambazi Tshs. 800/= Marie Monsen
Kitabu kinachoeleza ushuhuda wa mama mmoja aliyefanya kazi ya Umisheni katika nchi ya China wakati wa vita.
Lisha Kondoo Zangu Tshs. 400/= Fritz Larsen
Msaada kuandaa mahubiri kutoka Injili nne za Agano Jipya.
Msingi wa Imani Tshs. 700/= Carl Fr. Wisløff
Mwongozo wa elimu ya imani za Ukristo.
Msingi wa Wokovu Tshs. 900/= Øyvind Andersen
Utangulizi wa Waraka wa Warumi 1-8
Njia ya Wokovu Tshs. 300/= Kai Pedersen
Kijitabu kinachofafanua juu ya wokovu wa Yesu Kristo.
Mwonogzo wa elimu ya uchungaji wa kanisa. Kinapatikana kwa lugha ya kiingereza.
Labels: Masomo